TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma yafanikiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya Bil. 4,977,140,179 katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023.
Miongoni mwa miradi iliyofuatiliwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji katika vijiji vya Wilaya ya Tunduru yenye thamani ya Mil. 2,591,574,071, miundombinu ya barabara, madarasa wilaya ya Songea, Nyasa,Tunduru, Namtumbo na Mbinga yenye thamani ya 2,175,566,108 pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule za Sekondari katika Wilaya ya Nyasa na Namtumbo yenye thamani ya Mil. 210,000,000.
Hayo yamejiri katika kikao cha TAKUKURU Mkoa kilichofanyika leo tarehe 21 Agosti 2023 katika ofisi ya TAKUKURU na kuhudhuriwa na Waandishi wa Habari Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma ya utendaji kazi wa kipindi cha April hadi Juni 2023.
Akizungumza Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda alisema” katika ufuatiliaji wa miradi hiyo, miradi 5 yenye thamani ya shilingi 3,758,557,179 ilikutwa na mapungufu ambapo hatua mbalimbali zilichukuliwa ili kuondoa mapungufu hayo.”
Mwenda aliongeza kuwa, Kwa upande wa uchunguzi kumekuwa na malalamiko 28 kati ya malalamiko hayo malalamiko 16 yamehusishwa rushwa, katika sekta ya ardhi malalamiko 6, serikali za mitaa 02, afya 01, fedha 09, manunuzi 01, nishati 04, elimu 03 , na maji 01, pia taarifa 12 hazikuhusishwa rushwa.
Aidha, Kwa upande wa mashtaka alibainisha kuwa jumla ya kesi 04 zilifunguliwa ambapo kati ya hizo, kesi 03 zilikufunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Songea ambazo zimeisha na Jamhuri ilishinda kesi hizo na kesi 01bado inaendelea katika Mahakama ya wilaya Namtumbo.
TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma inaendelea kutekeleza mikakati ya utoaji wa Elimu kwa jamii juu ya Rushwa na madhara yake hususani katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, kwa lengo la kuzuwia mianya ya Rushwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo na Taasis za Umma na Taasis binafsi kwa kushirikiana na vijana wa Skauti kwa dhana ya kujenga uadilifu na uzalendo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa