Na;
AMINA PILLY
AFISA HABARI - MANISPAA YA SONGEA.
24.Novemba .2021
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Balozi Wilbert Ibuge amewataka wataalamu wa Manispaa ya Songea kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, uadilifu na uwazi ili kufanikisha utekelezaji wa miradi inayoendelea kujengwa.
Brigedia Ibuge ametoa pongezi hizo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya mpango wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambayo imefanyika leo tarehe 24 novemba 2021 na kufanikisha kutembelea miradi katika kata ya Mateka, Matogoro, Msamala, Mshangano, Lilambo, Mjimwema, na Lizaboni ambayo ipo hatua ya kuezekwa na lipu.
Alisema lengo la kutembelea miradi hiyo ni kutaka kukagua na kujiridhisha hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo na thamani ya fedha iliyotumika ambapo kwa manispaa ya Songea inatarajia kukamilisha na kukabidhiwa kwa mkuu wa Wilaya ya Songea ifikapo tarehe 10 disemba 2021.
Ametoa wito kwa wafanyabiashara wote Mkoani Ruvuma kuacha kupandisha bei ya vifaa vya ujenzi kwa lengo la kujinufaisha wao bila kujali uzalendo wa Taifa lao kwani Watoto wanaosoma katika shule hizo ni familia zao pia.
Alisema lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ikiwemo na kutoa huduma bora za afya, Elimu, miundombinu bora za barabara, na maji. Alibainisha.
Kwa upande wa Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea jumla ya Tshs 2,075,000,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Elimu miradi 26, na Afya ambapo kwasasa miradi yote ya Elimu (UVIKO 19) imefikia hatua ya kuezekwa na lipu.
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa miongoni mwa mikakati iliyowekwa ni pamoja na Kutoa mafunzo elekezi ya usimamizi wa miradi kwa kamati zote za ujenzi kwa kila taasisi, Kufanya kikao na wafanyabiashara ili kuwapatia msimamo wa Halmashauri juu ya uhakika malipo na kwa wakati na kutakiwa kusambaza vifaa vya ujenzi hadi eneo la mradi kabla ya malipo, na Kutoa bei elekezi kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi kama saruji, bati, tofali na nyinginezo.
Akibainisha baadhi ya chanagamoto zinazoikabili zoezi hilo ni pamoja na Wafanya biashara kupandisha bei ya vifaa vya ujenzi baada ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi kwa bidhaa za tofali ambazo hapo awali kabla ya mradi kuanza ilikuwa ni Tshs. 1500 hadi 1700, pia bidhaa za bati ilikuwa Tshs. 31,000 kabla ya kuanza kwa mradi na hatimaye ikaongezeka hadi Tshs. 33,000.
Akitoa shukrani za dhati kwa Kwa niaba ya Wananchi wa Manispaa ya Songea, alisema “kwa namna ya kipekee kabisa tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutupatia fedha za ili kuweza kutekeleza miradi hii ambayo itasaidia kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Halmashauri ya Manispaa ya Songea hususani Afya na Elimu.
Kwa upande wa afya Manispaa ya Songea imeanza kutekeleza miradi ya ujenzi wa vituo vya afya vipya 3 vilivyopo kata ya Lilambo, Subira na Msamala ambapo imeanza kujenmgwa na kufikia hatua ya msingi ambapo miradi hiyo inajengwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa