Mkoa wa Ruvuma umejaliwa kuwa na jumla ya eneo ka kilometa za mraba 67,550 kati ya hizo kilometa 63,968 ni ardhi na kilometa 3,582 ni maji yanayojumuisha ziwa Nyasa,mito na mabwawa.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe analitaja eneo la misitu ya asili ya miombo ni kilometa 41,567 sawa na asilimia 65 ya eneo lote la ardhi na kwamba misitu ya hifadhi ya serikali kuu ina eneo la kilometa 6,958,Halmashauri zina kilometa 170 na hifadhi za vijiji zina eneo la hekta 116,490.31.
Anabainisha kuwa jumla ya misitu yenye eneo la kilometa za mraba 41,507 zilizopo katika mkoa wa Ruvuma zinahusisha msitu wa Mhuwesi lenye ukubwa wa hekta 170,000,Mwambesi hekta 104,052,Sasawala hekta 39,424,Matogoro A hekta 32,900 na Matogoro B lenye hekta 7,128 .
Miongoni mwa vivutio adimu ni uoto wa asili ya jamii ya miombo ambao bado haujaharibiwa umekuwa kivutio adimu kwa wanyamapori,ndege,wadudu na viumbe wengine waliopo katika mapori ya akiba ya Selous, Liparamba na Gesimasoa.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 14,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa