Katibu tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewataka wananchi kutunza mazingira ili uoto wa asili uweze kuimarika.
Kauli hiyo imetamkwa wakati wa uzinduzi wa upandaji wa miti uliofanyika tarehe 07 machi 2025 katika shule ya sekondari Muungano Ruhuwiko ambayo inajengwa kwa Mil. 560 fedha kutoka Serikali kuu.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye zoezi hilo ambapo amewataka kupanda miti ya vivuri, miti ya matunda pia na kulinda mazingira ili miti iweze kukua.
Kwa upande wake afisa misitu manispaa ya Songea amesema katika uzinduzi huo wamepanda miti 3000 na wanatarajia kupanda miti 1,500,000 kwenye taasisi mbalimbali na wananchi.
Mwisho.
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa