MJI WA SONGEA UPO JUU YA MADINI
UTAFITI umebaini kuwa mji wa Songea na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Ruvuma yana utajiri wa madini mengi ya makaa ya mawe.Kuna kampuni za madini zimefanya tafiti na kubaini kuwa mkoa wa Ruvuma unaongoza nchini kwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini aina ya makaa ya mawe na chuma.
Katika utafiti huo unaonesha kuwa mji wa Songea upo juu ya madini ya makaa ya mawe ambapo mkoa wa Ruvuma unashika nafasi ya pili kwa uwingi wa madini ya dhahabu, nafasi ya kwanza inashikwa na mkoa wa Shinyanga na kwamba madini ya chuma ambayo yameanzia Liganga na madini ya makaa ya mawe yalioanzia Mchuchuma yamesambaa na kuenea katika eneo kubwa la mkoa wa Ruvuma.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa