Mkuu wa Wilaya Songea Pololet Kamando Mgema amekabidhi Mkataba wa lishe kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, mkataba ambao umesainiwa pande kuu mbili kati ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkataba ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka nane 8 kuanzia tarehe 01 Julai 2022 hadi tarehe 30 Juni 2030.
Kulingana na malengo na shabaha zilizoainishwa katika mikakati ya kitaifa ya muda mfupi, muda wa kati pamoja na muda mrefu ambayo nisehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwiaka mitano 5 pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala na Sera mbambali za nchi.
Utapiamlo unasababishwa na lishe duni, maradhi ya maramara, huduma hafifu za malezi na makuzi ya awali ya watoto wadogo, vifo na maendeleo ya akili kwa watoto ambapo katika kukabiliana na changamoto hiyo Serikali imeweka mpango madhubuti wa kuhakikisha kila Halmshauri, kata, na mtaa inasaini mkataba kwa lengo la kuleta mabadiliko katika kuboresha hali ya lishe ngazi ya jamii.
Aidha, zoezi la kusaini Mkataba wa lishe kwa Manispaa ya Songea limetekelezwa jana tarehe 25 Oktoba 2022 lililofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea kwa lengo la kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika Halmshauri, Kata na Mtaa na kuhakikisha kila mtendaji anasimamia ipasavyo utekelezaji wa afua za lishe.
Akizungumza na Maafisa watendaji kata, Pololet alisema “kila afisa mtendaji kata na mtaa ahakikishe anasimamia vigezo vya upimaji na vipaumbele vya kata kwa kila mwaka ambavyo ni pamoja na upatikanaji wa wa taarifa za hali ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano, kufanya ufuatiliaji wa watoto walioacha matibabu ya utapiamlo kwa kushirikiana na watoa huduma za afya ngazi yajamii.” Alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka wataalamu wa afya na maafisa watendaji kata na Mitaa kuhakikisha wanatekeleza mpango kazi wa utekelezaji wa lishe ambao utawezesha kutatua changamoto za watoto wenye utapiamlo mkali kwa kuwatembelea kwenye kaya zao kwa lengo la kutoa elimu na kupata taarifa halisi za walengwa.
Naye afisa lishe Manispaa ya Songea Frolentine kisaka amesema hali halisi ya utapiamlo mkali 0.2%, uzito uliozidi kwa watoto ni 2.5%, watoto waliozaliwa na uzito chini ya 2.5kg ni 6.5%, upungufu wa damu (anemia) kwa wajawazito 1.6%.
AMINA PILLY.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa