MKUU Mpya wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametangaza vita ya kupambana na mimba za utotoni katika mkoa wa Ruvuma.Akizungumza na wananchi wa Kata ya Majengo katika Manispaa ya Songea Mndeme amesema kampeni ya kupambana na ndoa na mimba za utotoni ni muhimu ili kufikia malengo ya kumkomboa mtoto wa kike na kumuweka katika mazingira salama ya kumuwezesha kufikia ndoto zake badala ya kukatizwa na mimba za utotoni.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anautaja mkakati anaotarajia kuutumia hivi sasa ni ule unaojulikana kama magauni manne ambao unamwezesha mtoto wake kujiamini na kufikia malengo yake.
Kwa mujibu wa Mndeme magauni hayo manne ameyataja kuwa ni gauni la kwanza mtoto wa kike kuwa ndani ya sare ya shule, gauni la pili ni la kuhitimu masomo,gauni la tatu ni la harusi na gauni la nne ni la kuvaa wakati wa ujauzito ambapo mtoto wa kike aatakuwa ametimiza ndoto zake.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa