MKURUGENZI wa Hamashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Tina Sekambo amefanya vikao siku tatu mfululizo na wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wakusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine yaani POS lengo likiwa ni kuweka mikakati mizito ya kuhakikisha mapato ya Halmashauri hiyo yanakusanywa kwa usimamizi wa kutosha ili kuhakikisha hakuna mapato yanayopotea au kuvuja.
Sekambo ameamua kufanya vikao hivyo kufuatia mapato ya Halmashauri kuonekana yameshuka katika mwezi huu hivyo ameagiza kila Mkuu wa Idara na vitengo vinavyohusika na ukusanyaji wa mapato kusimamia POS zote ili kuhakikisha kuwa mapato ya Halmashauri hiyo yanapanda.
Sekambo ameagiza kitengo cha TEHAMA,,watendaji wa mapato na Idara ya fedha sasa kufanyakazi kwa pamoja yaani Team work ili kuhakikisha POS zote zinakusanya mapato wakati wote na kwamba pasiwepo na kisingizio cha POS kuharibika au kupotea ambapo ameagiza yeyote ambaye atafanya uzembe wa aina yeyote hata sita kuchukua hatua za kisheria ikiwepo kulipa fedha zote ambazo zitakuwa zimepotea kwa uzembe.
Amewataka wakusanyaji hao kwenda kila mahali ambako wafanyabiashara wameweka bidhaa zao kwenda kukusanya mapato ambapo ameagiza kila Mkuu wa Idara kutambua POS zake na kiasi cha fedha ambazo zinakusanywa kwa siku kuhakikisha zinaingia katika Halmashauri na kwamba siku ya Alhamisi ambayo ni maalum kwa ukaguzi wa POS kila mkuu wa idara asimamie na kuhakikisha fedha zinapelekwa Benki.
"Wote mnaotumia POS hakikisheni mnafuata maelekezo ambayo mlipewa kabla ya kuanza kazi ,ikiwemo kutozima data za POS na kuacha kubonyesha mara mbili mashine ya print ambayo itasoma mara mbili,kuanzia sasa mkusanyaji yeyote ambaye atabonyesha mara mbili POS yake atalipia gharama hiyo,fuata ulichofundishwa kabla ya kuanza kutumia mashine uliopewa'',alisisitiza Sekambo.
Hata hivyo amesema wakusanyaji wote wanaodaiwa wanatakiwa kurudisha fedha hizo ambapo wataalam wa Manispaa yaani CMT wametoa hadi Oktoba 4 mwaka huu wakusanyaji wote wanaodaiwa na Halmashauri wawe wamelipa madeni yao na kwamba kuanzia sasa Halmashauri itaanza kuchukua hatua kwa wanaoisababishia Halmashauri hasara ikiwemo kuwaondoa katika kazi ya ukusanyaji wa mapato na kulipa fedha wanazodaiwa.Halmashauri ya Manispa ya Songea imenunua POS zaidi ya 100.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 23,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa