Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
28.10.2021
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka wakuu wa shule kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Mpango wa maendeleo ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO – 19, Fedha kutoka Serikali kuu chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muuungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kiasi cha Shilingi 660,000,000 .
Dkt.Sagamiko ametoa rai hiyo katika kikao kazi kilichoshirikisha Wafanyabiashara mbalimbali wa vifaa vya ujenzi, Wakuu wa shule, pamoja na wataalamu mbalimbali kilichofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kutoa maelekezo kwa wasimamizi wa miradi ya ujenzi pamoja na kuwaunganisha na wafanyabiashara ili kurahisisha usambazaji wa vifaa vya ujenzi kwa wakati na kwa kufuata utaratibu wa manunuzi ya fedha za Serikali.
Alisema miradi yote inatakiwa kukamilika mara ifikapo tarehe 15 disemba 2021 ambapo amesisitiza kila msimamizi wa mradi wanatakiwa kufanyakazi kwa kufuata miongozo na taratibu ziliwekwa kwa kuzingatia uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji.
Kwa upande wa wafanyabiashara wametoa maoni yao kwa kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kwa kuweka utaratibu mzuri ambao umewafanya wajenge mahusiano bora na wasimamizi wa miradi na wamemhakikishia kuwa watatoa huduma hizo kwa kufuata taratibu za manunuzi ya bidhaa za Serikali ikiwemo na kusambaza vifaa kwenye miradi kwa wakati.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa