NI AIBU kuona baadhi kiongozi wanapeleka kuuza mahindi kwa tapeli badala ya kuuza mahindi yako kwa kufuata mfumo sahihi uliowekwa na Serikali badala yake unauza mazao yako kwa njia isiyo sahihi, unaacha kuchukua hatua za haraka kudhibiti tatizo badala yake unasubili wananchi waumie kisha mnaleta ngazi ya juu. Hilo halikubaliki.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu Wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiwa katika kikao kazi na Maafisa Watendaji wa kata Mkoani Ruvuma, wakuu wa Wilaya wote, wakurugenzi wa Halmashauri zote, na viongozi mbalimbali wa ngazi ya kata kilichofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Bombambili 18 disemba 2020.
Mndeme alisema lengo kuu la kikao hicho ni kukumbushana juu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025 ikiwa inaelekeza kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato, uwezeshaji wa wananchi kiuchumi mikopo kwa wanawake, vijana, na walemavu inatolewa kwa walengwa sio makundi hewa.
Amewataka viongozi hao kusimamia upatikanaji wa bei sahihi ya saruji ambayo bei elekezi ya serikali kwa sasa ni shilingi 14,500/=, pamoja na bei elekezi ya pembejeo kwa wakulima. Amewaasa wale wote wenye tabia ya kuhujumu uchumi na wanaoficha saruji wachukuliwe hatua za kisheria.
Pongezi nyingi ziwafkie wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa kuongoza kitaifa uzalishaji wa mazao ya chakula hivyo ameawataka maafisa kilimo wote kusimamia na kutoa elimu kwa wakulima ili wananchi wapate kulima kilimo chenye tija. Hatimaye wananchi waweze kunufaika na mazao yao kwa kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuachana na kuuza mazao yao kwa matapeli kama Christopher Njako ambaye amewatapeli wakulima. Amesema Mndeme.
Amesema tapeli Njako amekamatwa pamoja na wasaidizi wake wote na ameshitakiwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi, na utakatishaji fedha. Hivyo ameawataka watendaji hao kusimamia ulinzi na usalama kwenye maeneo yao ya kazi hasa vijiji au mitaa ambayo ipo mpakani.
Mndeme amewataka watendaji hao kusimamia ukamilishaji wa miundombinu ya elimu ikiwemo madarasa, madawati, viti, meza, vyoo, maabara, mabawalo ili kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na shule wanapata mazingira mazuri ya kujifunzia.
Aidha, Wale wote watakao shindwa kupeleka watoto wao shule iwe darasa la kwanza, awali, au kidato cha kwanza wachukuliwe hatua za kisheria. “ Mndeme amesisitiza.”
Naye Mwenyekiti wa Watendaji Mkoa wa Ruvuma Bakari Kawina akizungumza kwaniaba ya Watendaji hao amesema “ wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa katika kikao hicho na alimpogeza kiongozi huyo kwa kufanya kikao cha kazi cha pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata Mkoani Ruvuma ambapo inawasaidia kuwaweka karibu na inawajengea uwezo wa kiutendaji kwa kupata uzoefu wa kiutendaji kutoka kwa wengine.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
19 disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa