Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amepokea kwa masikitiko taarifa rasmi ya kifo cha Mhe. Jenista Mhagama, Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri Mstaafu wa Afya.
Katika taarifa yake, Mkuu wa Mkoa amesema watamkumbuka Mhe. Mhagama kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika sekta ya afya, elimu na miundombinu. Amesema taratibu za kumhifadhi marehemu zimeshaanza kufanyika mkoani Dodoma, na baada ya mwili kuagwa rasmi Dodoma, taratibu nyingine zitafuata kwa kushirikiana na familia na viongozi wa wilaya na mkoa.
Mkuu wa Mkoa pia ametangaza ratiba ya mazishi na shughuli zinazohusiana na kumbukumbu za marehemu kama zifuatazo:
Mkuu wa Mkoa amewaomba wananchi kuungana na kushirikiana katika kipindi hiki na kumsindikiza marehemu katika safari yake ya mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa