Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameipongeza Ofis ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la Railway Children Africa (RCA) kwa kuleta mradi wa uanzishwaji wa Dawati ls Ustawi wa jamii katika Stendi ya mabasi Songea Mkoani Ruvuma.
Kanali Abbas alisema Mkoa wa Ruvuma ni kama Mikoa mingine ambapo unakabiliwa na changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani hususani Manispaa ya Songea,
Alibainisha kuwa changamoto hiyo husababisha watoto hao kujifunza na kujiingiza kwenye tabia hatarishi zaidi na wakati mwingine wanaweza kutumwa na watu wazima katika matukio ya wizi, uporaji, biashara ya ngono, ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha katika Manispaa ya Songea kuna ongezeko kubwa la watoto wanaotumiwa katika uuzaji wa bidhaa kama vifungashio katika maeneo ya masoko, wakiuza karanga,mayai,na korosho ambapo hali hiyo hufanya watoto wengi kuwa katika kufanyiwa vitendo vya ukatili na kuhatarisha ustawi wao.
Aliongeza kuwa uanzishwaji wa Dawati la ustawi jamii katika stendi kuu ya mabasi kupitia mradi huo utawasaidia kuwabaini watoto wanaoingia kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma na mikoa jirani.
Mradi huo utaweza kufanya kazi katika stendi ya Mabasi ya Manispaa ya Songea katika kipindi cha mwaka 2026, hivyo amewataka kusimamia na kutekeleza wajibu wa kuhakikisha huduma zitolewazo kupitia mradi huo zinakuwa endelevu. Alisisitiza
Akizungumza Kaimu wa Mganga Mkuu Mkoa wa Ruvuma Hilda Ndambalilo alisema lengo la mradi huu ni kuimarisha usala wa mtoto hususani watoto wa mtaani, kujumuisha wadau katika kuhakikisha usalama wao, Kuwaunganisha watoto na wazazi wao ili waweze kutunzwa na kutimiza ndoto zao.
Akizungumza Afisa Ustawi wa jamii Mkoa wa Ruvuma Victor Nyenza alisema mradi utalenga katika eneo la Stendi kuu ya mabasi ya Songea kwa lengo la kuwasaidi watoto waweze kuibua na kubaini changamoto za watoto waishio mtaani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa