MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amewaongoza wakazi wa Kata ya Matarawe Manispaa ya Songea katika kufanya usafi wa Mazingira Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi Julai.
Akizungumza baada ya kazi ya usafi kukamilika,amesema hajafurahishwa na kitendo cha wanaume kutokufanya usafi na kusema usafi ni jambo jema kwa kila mtu ili kuhakikisha tunatokomeza magonjwa yanayotokana na uchafu.
“Usafi unasaidia kupunguza magonjwa ya kipindupindu ili kuhakikisha Taifa letu linakaa katika mazingira salama na kazi ya watendaji ni kuhakikisha wanawapangia maeneo wananchi ya kufanyia usafi”.amesema Mgema.
Awali Wananchi wa Matarawe walitoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya wakidai gari taka kuchukua muda mrefu kufika katika eneo lao.
Akijibu kero hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo aliitaja changamoto inayosababisha magari ya kubebea taka kuchelewa kuwa baadhi ya magari yanakuwa mabovu,hata hivyo amewaahidi wakazi kuwa ofisi yake itayatafutia ufumbuzi changamoto ya ubovu wa magari inayochangiwa na kuchelewa kufunguka kwa mifumo.
Imeandikwa na Farida Musa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa