MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile, ameanza ziara ya kutembelea Kata kwa kata kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazohusu jamii ya kata husika.
Ziara hiyo imeanza tarehe 11 julai 2023 ambapo ameweza kutembelea kata ya Ruvuma ambako amekutana na wananchi na kuzungumza nao juu ya maendeleo ya kata na namna ya kutatua changamoto zao. Wakizungumza wananchi wa kata hiyo ambapo walisema changamoto kubwa ambayo inaikabili kata hiyo ni pamoja na kivuko, pamoja na Barabara.
Akijibu hoja hizo Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema kupitia mwaka wa fedha 2023/2024 Kata ya Ruvuma itatengenezwa barabara ya kiwango cha Lami kuanzia kata ya Majengo Hadi Kituo cha Afya Ruvuma.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa