• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKUU wa Wilaya ya Songea afanya utalii wa ndani katika kimondo cha Mbozi

Tarehe ya kuwekwa: June 30th, 2019

MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amefanya utalii wa ndani katika nyotamkia au kimondo kilichoanguka mwaka 1840 katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi mkoani Songwe.Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imefungua milango ya utalii katika ukanda wa kusini ili kuona serikali na wananchi katika mikoa hiyo inanufaika na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika maeneo hayo.

Hiki ni moja ya vivutio adimu vya utalii nchini ambacho kinawashangaza wengi. Kimondo hiki kilianguka mwaka 1840 katika kijiji cha Ndolezi Wilaya ya Mbozi.Km 62 kutoka Mbeya mjini kabla ya mji wa Mlowo na Vwawa kuna kijiji kinaitwa Mahenje. Kijiji hiki ndio njia panda ya kuelekea kwenye kimondo kijiji cha NDOLEZI kata ya MLANGALI km 12 kutoka barabara kuu ya lami.
 
 Kimondo hiki kinakadiliwa kuwa ndo kimondo kikongwe zaidi kati ya vile vilivyopo sasa duniani. Kina mchanganyiko wa madini mbali mbali kama vile Chuma 90%, Nickel 8%, Copa,salfa na Phosforasi 2%.Hiki kimondo ni cha nne kwa uzito kikiwa na tani 12, cha kwanza chenye uzito wa tani 60 kiko nchini NAMIBIA. Nchi zingine zenye vimondo ni Marekani, Green Land Magharibi, Mexico na Argentina.
 
 Kimondo hiki kwa mara ya kwanza kilivumbuliwa na mwenyeji wa maeneo hayo aliyekuwa muhunzi, alidhani ni jiwe la Chuma lakini alipojaribu kulikata alipata ugumu ambao ulimshangaza zaidi. Muhunzu huyu  ambaye alitoa taarifa kwa Chifu wao.Baada ya Chifu kushuhudia lile jiwe la ajabu aliwambia watu wake kuwa ile ilikuwa ni Baraka za Mungu kwa jamii yake hivyo walianza kutambika kukizunguka kile kimondo.
 
 Ilipofika mwaka 1930 alikuja Mjerumani mmoja kutokea Afrika Kusini aliyeitwa William H. Chnot na akaomba wazawa wampeleke kwenye jiwe la maajabu na aligundua lile halikuwa jiwe kama wazawa walivyokuwa wakidhani. Aliomba serikali ya kikolini ya Ujerumani itume wataalamu wake wa miamba ili kufanya utafiti. Walikata kipande kidogo na wakakipeleka Uingereza kwenye maabara. Majibu yalirudi mwaka 1931 na kubaini kwamba kile ni kimondo.
 
 Kimondo hiki ni cha baridi wakati wote kutokana na mchanganyiko wa madini yake. Madini ya chuma kwa kawaida hupokea joto lakini madini ya Nickel hutawanya joto ndo maana ni cha baridi muda wote. Ingawa nickel ni asilimia 8 tu na chuma ni asilimia 90 lakini nickel yana nguvu kuliko chuma kwa kutawanya joto.


Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Bil. 22.9 Kujenga Masoko ya Kisasa Manzese A na B, na Kiwanda cha Kuchakata Mazao ya Nafaka Lilambo

    July 06, 2025
  • MBUNGE SONGEA MJINI AKABIDHI KOMPYUTA NA KUFADHILI UKARABATI WA OFISI ZA POLISI

    June 27, 2025
  • DC Songea bAzindua Dawati la Huduma za Ustawi wa Jamii Stendi ya Mabasi Songea

    June 24, 2025
  • Meya Mbano; Amewataka Wananchi Kulinda Haki za Watoto

    June 16, 2025
  • Tazama zote

Video

Makabidhiano ya Mkataba Soko la Manzese A&B
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa