MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka Waendesha Bodaboda na Bajaji kuhakikisha wanauunda umoja wao ili kuwezesha kuwa na Sauti moja wanapokuwa changamoto mbalimbali ambayo inapaswa kusikilizwa na viongozi husika.
Hayo yamejili wakati wa kikao kazi cha Mkuu wa Wilaya ya Songea na Waendesha Bodabda na Bajaji kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambacho kilishirikisha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, pamoja na uongozi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kusikiliza kero za Madereva hao.
Ndile alisema kuwa “ mnapokuwa na uongozi imara kupitia umoja wenu mtaweza kupeleka changamoto zenu kwenye Mamlaka husika kwa kufuata utaratibu unaokubalika ambao pia utawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo na kupata mikopo, kupata mafunzo ya Udereva kupitia VETA na kujenga mahusiano bora baina yao na Serikali.”
Amewataka kufuata sheria bila Shuruti ikiwemo na kulipa leseni ya Udereva na Leseni ya Chombo chenyewe pia kuwepo na utaratibu wa kukutana mara kwa mara ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa Upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Songea ASP Muya Zuberi Maunganya amewataka Waendesha Bajaji na Bodaboda kuendelea kufuata Sheria za Usalama Bararani ikiwemo kupata Leseni na kuzingatia Maegesho rasmi yaliyoruhusiwa na Mamlaka husika.
Kwa upande wa Waendesha Bodaboda na Bajaji walitoa Shukrani kwa Serikali kwa kuitisha kikao hicho ambacho imekuwa ni sehemu ya kutoa kero zao na kusikilizwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa