Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameawataka Wakurugenzi wa Halmashauri wenye miradi ya ujenzi wa madarasa kuhakikisha inakamilika kwa wakati kabla ya kufunguliwa kwa shule januari 11.2021.
Pololet ametoa agizo akiwa katika kikao cha kamati ya Ushauri Wilaya DCC, ambacho hushirikisha Wataalamu wa Halmashauri tatu ikiwemo na Madaba, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Manispaa ya Songea pamoja na Wadau mbalimbali wa Maendeleo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea jana 07 januari 2021.
Alisema lengo la kikao hicho ni kupokea ushauri mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi na kusaidia kuijenga Serikali yetu ili kuleta Mafanikio yenye tija kwa jamii ya Songea, na kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi katika kipindi cha 2019/2020.
Aliongeza kuwa, Serikali imeweka uwekezaji wa kituo kikuu cha mabasi Tanga kwa ajili ya kuongeza mapato na kugawa fulsa kwa wananchi wa Songea hususani wafanyabiashara kwa lengo la kuwainua kiuchumi.
Alisema “mabadiliko yoyote yanagharama pia lazima tutambue kuwa mabadiliko haya yanaleta fulsa kubwa ya kuendeleza mji wa Tanga na fulsa kwa wafanyabiashara , mama lishe, Bodaboda na wengineo kwahiyo msione kama ni jambo la ajabu au kwa ajili ya kuwanyanyasa wananchi hapana.” Nanukuu “Serikali inayoongozwa na Mh. Rais John Pombe Magufuli haipo tayari kuona wananchi wake wananyanyaswa “ Pololet alibainisha.
Amewataka wataalamu wa Manispaa ya Songea kuhakikisha stendi ndogo ya Ruhuwiko inaboreshwa haraka iwezekanavyo ili magari yaweze kuingia na kutoka kwa urahisi na usalama Zaidi.
Alitoa wito kwa wasimamizi wa vyombo vya moto ( usalama barabarani) kuhakikisha wanaimarisha ulinzi na usalama pamoja na kufanya uchunguzi kwa madereva wa boda boda ambao wanajihusisha kuwasafirisha abiria kwa kuwatoza nauli kubwa zaidi ya shilingi 15,000 kutoka mjini hadi Tanga kinyume na sheria, endapo watabainika wachukuliwe hatua za kisheria. Pololet ameagiza.
Alisema Serikali imetoa Tsh bilioni 6.8 kwa ajili ya ujenzi wa stendi ili iwanufaishe wananchi kwa ajili ya ya kuwaletea maendeleo yao kwahiyo stendi nilazima itumike ipasavyo.
Akiwahimiza wataalamu hao kila waaandaapo taarifa zao lazima iwekwe taarifa za mikopo iliyotolewa kwa kila kikundi ili kila mwananchi apate kufahamu serikali inawafanyia nini kwa kuzingatia ugawaji sahihi wa mikopo ili fedha zinazotolewa na Halmshauri ziwafikie walengwa kama vikundi vya wananawake 40%, vikundi vya Vijana 40%, na walemavu 20% Kwa ajili ya kuleta chachu ya Maendeleo kwa wananchi pamoja na uboreshaji wa huduma za afya kupitia vituo vya Afya.
Akizungumzia timu ya Maji maji ambapo alisema Zaidi ya miaka minne timu ya majimaji haijacheza ligi kuu ya Tanzania kutokana na kushuka kwa daraja, kutokana na tatizo hilo serikali imejipanga kuboresha timu ya majimaji kwa kuiongezea nguvu ikiwemo na kuchukua changamoto zao kuzipeleka ngazi ya mkoa ili timu hii itazamwe kimkoa Zaidi.
Naye Afisa misitu Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Chale alisema Jiolojia ni muonekanao wa kijiografia wa sehemu Fulani ambayo inahusisha miinuko, miamba, mabonde, mapango na maporomoko.
Chale aliongeza kuwa hifadhi ya jiolojia katika safu yamlima matogoro ipo chini ya usimamizi wa TFS, Serikali ya vijiji pamoja na Taasis zinazojihusisha uhifadhi wa milima ya matogoro kusini, milima ya matogoro mashariki, magharibi, mapambo yamlima matogoro A na Chandamali, utamaduni wa jamii wa wangoni na wandendeule, makumbusho tatu zilizoko Manispaa ya Songea, mabwawa ya umeme wa maji chipole, maporomoko ya maji nakatuta, msitu wa Chandamali, Mabwawa ya Soamaki Ruhila, na milima ya limamu na mpiganjuchi.
Alisema umuhimu wa kuhifadhi katika safu ya milima ya matogoro ni mkubwa kwa kuwa una vitu vingi vya umuhimu kwa ajili ya kizazi cha leo na kesho pia milima ya matogoro inatarajiwa kuwa nyenzo muhimu kwa kukuza pato la Wilaya na Mkoa kwa kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea hifadhi kwa kuongeza vivutio vya watalii. Pia watasaidaia watalii hao kununua vifaa vya kiutamaduni na kusaidia jamii kujiongezea kipato.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
08.Januari 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa