Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amezindua kampeni ya Dawa ya magonjwa ambayo yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele Mkoani Ruvuma.
Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema
Magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele ndani ya jamii, hasa jamii maskini, lakini
jamii yenyewe na wataalamu husika ama viongozi hawayapi umuhumu kulingana na madhara
yake katika jamii,magonjwa hayo ni Usubi, Matende, Mabusha, Trakoma, Kichocho na Minyoo
ya tumbo.
Mgema ameyataja madhara ya Magonjwa hayo maumivu ya muda mrefu na wakati
mwingine kusababisha ulemavu wa kudumu, Hudhoofisha ukuaji wa maendeleo ya mtoto
kimwili na kiakili, Magonjwa haya yasipotibiwa mapema huongeza maambukizi na hata
kusababisha kifo.
“inakadiriwa kuwa watu bilioni moja duniani kote tayari wameathirika na Zaidi ya bilioni mbili
wako hatarini kupata maambukizi ya magonjwa hayo. Nchini Tanzania wananchi wote, yaani
milioni 53, hivi sasa wapo hatarini kuambukizwa magonjwa haya. Inakadiriwa kuwa watu
milioni tano wameathirika kwa magonjwa hayo.” Amesema Mgema.
Hata hivyo, kwa Manispaa ya Songea tupo kwenye kampeni ya uwezeshaji wa dawa ya
MECTIZAN kwa ugonjwa wa Usubi, ndio ugonjwa unaopaswa kutolewa kingatiba kwa
wananchi wote wa Manispaa ya Songea, isipokuwa chini ya miaka mitano, mama wajawazito na
wagonjwa mahututi.
Ili kufanikisha kujikinga na magonjwa haya inabidi kutumia dawa za kutibu na kuzuia magonjwa
haya ambazo zinatolewa kila mwaka kwenye maeneo yaliyogundulika kuwa na ugonjwa,
kuzingatia usafi wa uso kwa kunawa angalau mara mbili kwa siku na usafi wa mwili kwa
ujumla, kuzingatia matumizi sahihi ya choo ,jiepushe kuoga /kuogelea na kutembea bila kuvaa
viatu kwenye maji yasiyo safi, kujikinga kuumwa na wadudu wanaosambaza ugonjwa huo,
kutibiwa mara baada yakuona dalili za ugonjwa na mwisho kutoa eilmu ya afya kwa jamii.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mameritha Basike
amesema magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa Manispaa ya Songea yamekuwa
yakipungua mwaka hadi mwaka pindi wanapo kunywa Dawa,
Ameyataja mafanikio na umuhimu wa kupata dawa hiyo kwa mwaka 2018 walikuwa na kesi 13
za ugonjwa wa usubi zilizoripotiwa ni sawa na asilimia 0.004 kati ya wagonjwa 295,010, mwaka
2019 Juni tulipata kesi 8 za ugonjwa wa usubi zilizoripotiwa ni sawa na asilimia 0.01kati ya
wagonjwa 150,648walio kuja kupata huduma ya tiba kwenye kituo.
Naye,Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Manispaa ya Songea Prodi Komba
amesema vimerea vya Usubi vinazaliwa kwenye maji yanayo kwenda kasi kwenye mistu ndio
maana serikali yetu kupitia wizara ya afya wameamua kumezasha Dawa za MECTIZAN kwa
ajili ya kinga tiba ya ugonjwa wa Usubi.
Kwa upande wake, Komba ametoa rai kwa watu ambao watachukua jukumu la ugawaji Dawa
wajitahidi kutoa ushauri kwa wananchi ambao utawaondoa hofu katika kumeza dawa hizo.
Meza dawa za kingatiba kila mwaka kuzuia magonjwa ya usubi, Matende na Mabusha,
Trakoma, Kichocho na Minyoo ya Tumbo.
Imeandaliwa na
Farida Musa
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 3, 2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa