Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amewataka wataalamu wa ujenzi kuhakikisha wanasimamia kwa ufanithi miradi ya ujenzi wa madarasa inayoendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali Wilayani humo na kufanikisha kukabidhi ifikapo tarehe 30 Novemba mwaka huu.
Ziara hiyo imefanyika jana tarehe 29 Oktoba 2022 kwa kufanikisha kutembelea ujenzi wa madarasa 76 katika shule za sekondari ambapo amefurahishwa kuona ujenzi ukiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, ukuta, renta, kuezeka na nyingine ukamilishaji.
Mhe. Pololet amesema Wilaya ya Songea inaendelea na ujenzi wa madarasa 96 kati ya hayo madarasa 76 yanajengwa Manispaa ya Songea, Madarasa 10 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, na madarasa 10 Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Ametoa pongeazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Bil. 1.52 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, ambapo amewarai wataalamu, na kamati za ujenzi kwa kuendelea kushirikiana na kuhakikisha inakamilika na kukabidhi ifikapo tareghe 30 Novemba
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa