HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo Machi 24,2018 imeuza kwa njia ya mnada wa hadhara mitambo yake 16 ikiwemo magari,Pikipiki na mitambo mingine chakavu na kufanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 87.75.
Mitambo ambayo imeuzwa katika mnada huo ni Mitsubishi Bozer ,Toyota land cruser station wagon mbili,Nissan station wagon,,Nissan station wagaon tipper,Isuzu tipper mbili,Hyster Roller,pikipiki sita aina ya Suzuki 125,pikipiki aina ya Honda 110 na Hysosung.
Hata hivyo fedha taslimu ambazo zimekusanywa katika mnada huo uliofanyika katika Karakana ya Manispaa ya songea na kusimamiwa na YONO AUCTION MART chini ya Dalali Mahiri Zuberi Lumbizi ni shilingi zaidi ya milioni 26.
Kiasi hicho cha fedha taslimu kilichopatikana ni moja ya masharti ya mnada ambapo Mnunuzi alitakiwa kulipa amana ya fedha taslimu si chini ya asilimia 25 ya thamani ya gari,Pikipiki au mtambo atakaoununua na kukamilisha malipo yote katika muda wa siku 28 kuanzia tarehe ya mnada.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea<%2
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa