Hawa Hassan(57) mkazi wa mtaa Pachanne,kata ya Mjimwema anasema kabla ya kuanza kupata ruzuku ya shilingi 36,000 kutoka TASAF alikuwa anaishi katika mazingira magumu kwa kuwa mume wake alimuacha mara ya baada ya kupata maradhi ya miguu.
Amesema kutokana na ruzuku hiyo aliamua kuanza biashara ya ndogo ndogo ya kuuza mafuta ya kula na nyanya, na kucheza upato hivyo kufanikiwa kupata shilingi laki moja Machi 2016 ambazo zilimwezesha kununua kuku wa mayai 74 ambazo zimemletea faida kubwa ikiwemo kujenga nyumba nyingine mpya yenye vyumba vitatu.
Hawa anasema hivi sasa ana uhakika wa maisha, kwa kuwa mradi wake wa kuku unaendelea vizuri.Hata hivyo amesema hivi sasa amebakiwa na kuku wa mayai 47 ambao wanaendelea kumsaidia katika maisha yake na familia
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa