MRADI WA BUSTANI WA KISASA MANISPAA YA SONGEA
UJENZI wa bustani ya kisasa ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao utabadilisha muonekano wa Manispaa hiyo,umeanza katika eneo ambalo lipo kati kati ya viunga vya mji wa Songea.
Mradi huu ambao utachukua miezi sita hadi kukamilika ni miongoni mwa miradi ambayo inafadhiliwa na Benki ya Dunia ambao unatarajia kugharimu sh.milioni 399.
Ramani ya mradi huu wa aina yake katika mji wa Songea inaonesha kuwa utazungukwa na eneo la kulipia kwa ajili ya kuegesha magari,vyoo vya kulipia na vibanda vya kupumzikia.
Mradi huu pia utakuwa na maeneo kwa ajili ya kuchezea watoto,hoteli kwa ajli ya kupata chakula na vunywaji.Mradi huu pia unatarajiwa kuwa na eneo maalum la kupata taarifa za uwekezaji na utalii katika manispaa na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Jambo la kufurahisha ni kwamba Bustani hiyo itapandwa miti na nyasi ambazo zinaongeza mandhari nzuri na muonekano wa kuvutia wa Manispaa ya Songea kwa kuwa bustani hiyo ipo kati kati ya mji wa Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa