Ujenzi wa barabara hizi ulianza Julai mosi,2015 na ulitarajiwa kukamilika Juni 30,2016.Mradi huu umetekelezwa na Wakandarasi wawili, ambapo mara ya kwanza ujenzi ulifanywa na Mkandarasi M/S Lukolo Company LTD aliyeingia mkataba na Halmashauri wa kujenga KM 8.6 za barabara kwa kiwango cha lami nzito kwa gharama ya shilingi 14,320,586,464.39 ikijumlishwa na VAT.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo amesema gharama hiyo ya mkataba ilifanyiwa mapitio(revised contract ) na kufikia Tshs 11,933,899,897.09 ikijumlishwa na VAT.
“Muda wa Mkataba ulikuwa ni miezi 24, ambapo mkataba ulivunjwa tarehe 09/10/2017 baada ya Mkandarasi kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati kulingana na mkataba’’,amesema Sekambo.
Hata hivyo amesema Mpaka Mkataba unavunjwa Mkandarasi alikuwa amelipwa jumla ya Tshs 4,352,975,711.70 kati ya fedha hizo malipo halisi ya Mkandarasi yalikuwa Tshs 2,204,887,742.04 na malipo ya awali (advance payment) yalikuwa Tshs 2,148,087,969.66 .
Amesema kati ya fedha hizo za malipo ya awali, Mkandarasi alikuwa anadaiwa Tshs 1,597,006,612.99, fedha hizo zote zimerudishwa na Bank of Africa tarehe 14/12/2018. Hadi mkataba unavunjwa kazi ilikuwa zimefikia hatua mbalimbali.
Kulingana na Sekambo,ujenzi wa barabara mara ya pili, ulianza Machi 25,2018 baada ya kazi kutangazwa upya na kumpata Mkandarasi CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CORPORATION (SIETCO) ambaye alitarajiwa kukamilisha mradi Septemba 30,2019 ambapo Mhandisi Mshauri wa mradi huu ni HOWARD HUMHFREYS (T) LTD.
“Ujenzi huu unahusisha barabara za FFU –Matogoro - KM.3.2,Songea girls – Mateka KM 1.5,Bombambili – Mwembechai KM 2.5,Majengo Mitumbani – Yapenda Annex. KM 1.0,Stendi ya Mlilayoyo - Polisi Station. KM 0.4,Matomondo - planet bar. KM. 0.8 na Buhemba Annex - Kalembo KM 0.9’’,amesema.
Kazi zinazofanyika katika ujenzi wa barabara ni,Kujenga barabara katika kiwango cha lami nzito zenye urefu wa KM 10.3 na upana wa Mita 8,Kujenga mifereji,Kujenga njia za watembea kwa miguu, Kuweka taa za barabarani,Kujenga Maabara kwa ajili ya kupima sampuli za udongo, Zege na baadhi ya sampuli za lami,(Material Test)
Mradi huu mpaka kukamilika utagharimu jumla ya Tshs 13,164,965,966 na gharama ya Mhandisi mshauri ni Tshs 337,000,000.
Mpaka sasa mradi kwa ujumla umefikia asilimia 90 ya utekelezaji . Mradi huu baada ya kukamilika kwa asilimia 100 utapandisha hadhi ya Manispaa na utarahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao, bidhaa na abiria kutoka katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hivyo kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Manispaa na Wakazi wake. Pia barabara hizi zitasaidia kupunguza msongamano wa magari na pikipiki katikati ya Manispaa hivyo kupunguza muda wa kuwa barabarani.
Mradi huu unaongeza thamani ya Ardhi na nyumba zilizopo pembeni mwa barabara.Barabara zinazojengwa zitawekewa taa za barabarani ambazo zitasaidia katika ulinzi na usalama wakati wa usiku hivyo kupunguza matukio ya uhalifu kwa Raia na mali zao. Pia taa zitawasaidia wafanyabiashara wadogo kuongeza muda wa kukufanya biashara zao wakati wa usiku na hivyo kuongeza kipato na mzunguko wa fedha ndani ya Manispaa.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 30,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa