Mradi wa ujenzi wa Stendi ya mabasi katika kata ya Tanga Manispaa ya Songea mkoani
Mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kisasa katika kata ya Tanga Maispaa ya Songea unafanywa na Kampuni ya China Sichuan International.mradi umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2019.Mradi huu katika awamu ya kwanza unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikia asilimia 45 hadi kufikia Desmba 2018.
Kazi ambazo zinafanyika katika awamu ya kwanza katika stendi hii ni ujenzi wa lami nzito yenye kilometa mbili,taa barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya tiketi,jengo la utawala,vyoo vya matundu 12 na eneo la kupaki magari.Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya shilingi bilioni sita.
Mradi huu hadi kukamilika katika awamu mbili unatarajia kugharimu shilingi bilioni 12 ambapo katika awamu ya kwanza, zitatumika shilingi bilioni sita na kwamba stendi mpya ya mabasi inatarajia kuanza kazi baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji ambayo ni kuanzia Oktoba 2019.
Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa mji,Manispaa ya Songea iliamua kutenga eneo la kujenga kituo kikuu cha mabasi katika Kata ya Tanga ikiwa ni umbali wa takribani kilometa 14 toka mjini Songea.Kazi nyingine ambazo zitafanyika katika awamu ya kwanza na pili ya mradi huo ni kujenga barabara za kuingia na kutoka stendi zenye kiwango cha lami nzito,kujenga mirefeji ambayo itapeleka maji mtoni,ujenzi wa eneo la stendi lenye ukubwa wa meta za mraba 32,914,kuweka taa za barabarani katika eneo lote la stendi,eneo la utawala na kujenga majengo yenye hoteli za kisasa.
Ruvuma umefikia asilimia 45.Mradi huu unatekelezwa na Kampuni ya China Sichuan International (SIETICO) .Mradi huu ni wa miezi 18 ambao umeanza Machi 2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa