Matukio ya mara kwa mara ya mamba kuua watu mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma lilikuwa ni jambo ambalo liliwatia hofu wakazi wa mwambao mwa ziwa Nyasa katika kipindi cha miaka ya 90.
Hata hivyo matukio ya watu kukamatwa na kuuawa na mamba katika ziwa Nyasa yamepungua ukilinganisha na kipindi cha kati ya mwaka 1990 na 2005 ambapo mamba walikamata hadi mzungu katika eneo la Liuli .
Matukio ya mamba kuua watu yalipungua baada ya kujitosa kwa askari Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Watanzania(JWTZ) ambaye hivi sasa ni marehemu John Mpembo maarufu kwa jina la Mrema ambaye alifanya operesheni kabambe ya kuwaua mamba kwa kutumia mtego maalum na kufanikiwa kuwaua mamba wanaokadiriwa kuwa kati ya 600 hadi 800.
Mrema aliomba kibali cha kuua mamba kutoka,Wizara ya Malisili na Utalii baada ya vitendo vya mamba hao kukamata watu kuongezeka na kuleta hofu kwa wananchi mwambao mwa ziwa Nyasa.
Joseph Ndomondo ni Mpwa wa Mzee Mrema ambaye anakiri ni kweli mzee Mrema alifanikiwa kuua idadi kubwa ya mamba wala watu hali ambayo imesabaisha vitendo vya mamba kukamata watu katika ziwa Nyasa kupungua.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa