Mto Ruvuma ni miongoni mwa mito maarufu barani Afrika na duniani kwa ujumla wake.Chanzo cha mto huo kipo Manispaa ya Songea katika msitu wa serikali uliopo katika milima ya Matogoro.
Mto Ruvuma unamwaga maji yake katika Bahari ya Hindi kwenye eneo la kati ya Mtwara nchini Tanzania na Rasi ya Delgado nchini Msumbiji.
Chanzo hicho adimu ni kivutio adimu na cha kipekee cha utalii katika Manispaa ya Songea ambacho kinavutia wengi wanaotembelea hapo.
Msitu wa serikali wa Matogoro pia ni chanzo cha mito ya Ruegu ambao unachangia asilimia 19 ya maji katika Mto Rufiji ambao unamwaga maji yake Bahari ya Hindi.
Msitu wa Matogoro pia ni chanzo cha Mto Luhira ambao unaungana na mto Hanga kutengeneza mto Ruhuhu ambao unachangia asilimia 20 ya maji katika ziwa Nyasa.
Kwa hiyo milima ya matogoro ni chanzo cha mito mitatu mikubwa nchini ambayo ni mto Ruvuma,Rufiji na Ruhuhu.
Hifadhi ya Msitu wa milima ya Matogoro ilianzishwa miaka ya 1950 ikiwa na hekari 2259 za miti ya kupandwa.Msitu wa milima ya Matogoro kisheria upo chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na ulitangazwa katika gazeti la serikali ya kikoloni mwaka 1951.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manipaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa