Mstahiki Manispaa ya Songea Michael Mbano, akabidhi mahitaji ya FUTARI kwa viongozi wa BAKWATA Wilaya ya Songea kwa lengo la kuwafariji watu wenye mahitaji maalumu wa dhehebu la Kiislamu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu Ramadhani.
Miongoni mwa mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na mchele kilo 100, Mafuta lita 20, Tambi, unga wa ngano kilo 50, pamoja na Sukari kilo 50.
Mhe. Mbano, amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuwa na tabia ya kutoa mahitaji kwa wahitaji katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu ili kujenga upendo kwa jamii.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 18 Machi 2025 katika ofisi ya Mstahiki Meya Manispaa ya Songea.
Kwa upande wake Shekhe wa Wilaya ya Songea, Shekhe Ibrahimu Rashidi ameishukuru Manispaa ya Songea kwa zawadi zilizotolewa ambapo wameahidi kwenda kuwagawia watu wenye mahitaji wa kiislamu ambao wapo kwenye mfungo wa Ramadhani.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa