Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Pikipiki moja 1 kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kazi wa Maafisa Watendaji wa Kata ili kuwafikia wananchi na kutoa huduma kwa wakati.
Pongezi hizo zimetolewa leo 21 Februari 2023 na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano wakati wa kukabizi Pikipiki kwa Afisa Mtendaji wa Kata Subira, Alexanda Kapinga ambapo amemtaka kutumia pikipiki hiyo kwa ajili ya kuhudumia wananchi pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo.
Mhe. Mbano alisema Serikali itaendelea kuleta Pikipiki kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa kazi kwa Watendaji wa kata, ambapo kwa awamu ya kwanza Manispaa ya Songea imepokea Pikipiki moja 1 ambayo amekabidhiwa Mtendaji wa kata ya Subira kutokana na kata hiyo kuwa na umbali na hupelekea kutofikika kwa wakati kuliko kata nyingine.
Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Subira Alexanda Kapinga ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kumpatia kitendea kazi (usafir) ambao utamsaidia kufika ofisini kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa