Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe. Michael Mbano, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Meya Mbano ameeleza kuwa miradi mingi ya maendeleo imekamilika kwa wakati, jambo linaloonesha dhamira ya dhati ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.
Pato la Halmashauri limeongezeka kutoka shilingi bilioni 2.5 hadi kufikia bilioni 9, jambo linalodhihirisha ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa rasilimali.
Amewahimiza madiwani kuendelea kumsemea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kata zao kutokana na mafanikio yanayoonekana
Meya Mbano ametoa shukrani kwa viongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na wananchi kwa ushirikiano wao katika kipindi cha uongozi wake.
Taarifa hii imetolewa katika kikao cha robo ya tatu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe 30 Aprili 2025 kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIABO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa