HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea imepongezwa kwa kutozalisha madeni mapya kutoka kwa wazabuni na wadau mbalimbali ambapo wameitaka Halmashauri hiyo kuendelea kuwa safi bila ya kuwa na madeni mapya.
Rai hiyo imetolewa kwenye mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika tarehe 31 Julai 2024 ambao ulihudhuriwa na Madiwani, Wataalamu, Viongozi wa vyama vya siasa, pamoja na wananchi uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ikiwa ni kikao cha baraza la nne kwa mwaka 2023/2024.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amewataka Maafisa watendaji wa Kata wahakikishe wanasimamia utekelezaji wa zoezi la usafi wa mazingira sambamba na usafishaji maeneo yote ambayo yalilimwa mahindi wahakikishe yanaondolewa sambamba na wananchi kufungua njia/barabara zilizofungwa ili ziweze kupitika.
Alisema “ Mtakumbuka mwezi Juni 29 mwaka huu 2024 Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilipokea fedha zaidi ya Bil. 4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali fedha hizo, zinatakiwa kutumika kwenye miradi na kuhakikisha inakamilika ifikapo Septemba 30 mwaka huu, hivyo amewataka wataalamu kunasimamia miradi hiyo na ikamilike kwa wakati.” Mhe. Mbano alibainisha.
Amewataka wataalamu kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ambayo yatawezesha kutatua changamoto za Halmashauri ambapo kwa mwaka 2024/2025 kupitia mapato yake ya ndani ya Halmashauri imetenga bajeti ya kiasi cha Mil 200 kwa ajili ya utengenezaji madawati ya shule, hivyo amewasisitiza wataalamu hao kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato hayo.
Aidha amewashauri wataalamu wa Manispaa hiyo kuhakikisha wanashughulikia haraka mchakato wa mabadiliko ya Bendera ya Halmashauri haraka iwezekanavyo kabla ya kuanza kwa Uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa ili Bendera hizo ziweze kupeperushwa kwenye kila ofisi ya Serikali za Mitaa.
Akizungumza Katibu Tawala Wilaya ya Songea Ndugu. Mtella Mwampamba amewataka Maafisa maendeleo ya jamii kutumia njia iliyotumika kuelimisha jamii kuweza kukopa mkopo na njia hiyo hiyo itumike kudai madeni hayo ili kuweza kufanikiwa kukusanya madeni ya shilingi Bil. 1.3 fedha ambazo ni marejesho ya vikundi vya Vijana, wanawake na Walemavu ambazo hazijarejreshwa, hivyo amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuongeza jitihada za kukusanya fedha hizo ili ziweze kukopeshwa kwenye vikundi vingine vyenye sifa ya kupata mikopo.
Rai imetolewa kwenye Baraza hilo kutokana na kubadilika badilika kwa bei ya Mahindi, hivyo amewataka wananchi kuanzisha utaratibu wa kuuza unga na Pumba za mahindi badala ya kuuza mahindi pekee ili mkulima aweze kujipatia kipato.
Akizungumza Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea Mjini ndugu. James Mgego, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi pamoja na pongezi hizo, amewataka wataalamu kukamilisha miradi Viporo ili iweze kutumika kwa wakati sambamba na kumsemea Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na miradi yote iliyotekelezwa ili wananchi waweze kufahamu.
Akizunzungumza kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu ambapo alisema, amepokea maagizo yote yalitolewa na viongozi kupitia baraza la madiwani na kuahidi kusimamia ukusanyaji wa madeni ya vikundi shilingi Bil. 1.3 fedha zilizotolewa mikopo ya wananwake 4%, Vijana 4% na walemavu 2%,pia Maafisa watendaji kusimamia safi wa mazingira pamoja na ukuamilishaji wa miradi ya maendeleo. “Alibainisha”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa