MTI unaoaminika kuwa unaoongoza kwa ugumu na kuishi miaka mingi duniani umegundulika katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea
Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Majimaji Mhifadhi Kiongozi Barthazar Nyamusya anautaja mti huo kuwa unafahamika kwa jina la Chikunguti ambao ulitumika kama alama kwenye kaburi la shujaa wa vita ya Majimaji Nduna Songea Mbano ambaye aliuawa na kuzikwa mwaka 1906 mti huo ukiwa upo.
Inakadiriwa mti huo hivi sasa utakuwa na miaka zaidi ya 125 .Kulingana na Mhifadhi huyo aina hiyo ya miti Ina uwezo wa kuishi hadi miaka 1000.Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji akiwa katika kaburi la Songea aliuona mti huo na kusisitiza kuwa aina hiyo ya miti ndiyo miti migumu kuliko yote duniani na kwamba ina uwezo wa kuishi miaka mingi.
Karibu katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yaliopo mjini Songea kuna mengi ya kujifunza ikiwemo vivutio adimu vya utalii wa kiutamaduni na kishujaa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa