• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MTO Ndumbi unavyosababisha vifo na majeruhi Nyasa

Tarehe ya kuwekwa: May 9th, 2018

MTO Ndumbi uliopo katika Kijiji cha Mkili Kata ya Nindai Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma umekuwa unasababisha majanga kwa jamii ikiwemo kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu.

Afisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji hicho Nathan Kambanga amekiri mto huo ambao unamwaga maji yake ziwa Nyasa kipindi cha masika unapofurika umekuwa unasababisha athari kijamii na kiuchumi ikiwemo baadhi ya watu kupoteza maisha.

Esau Mwanja akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji hicho amedai kuwa hadi sasa tayari watu kumi wamepoteza maisha baada ya kusombwa na maji ya mto huo ambapo kuna watu kadhaa ambao wamepata ulemavu .

“Kumbukumbu zangu zinaonesha watu Zaidi ya kumi wamekufa katika mto huu na wengine kupata ulemavu,tunaomba serikali itujengee daraja ili kunusuru maisha ya watu wa mwambao mwa ziwa Nyasa’’,anasisitiza Mwanja.

Licha ya kusababisha vifo inadaiwa mto huo pia unasababisha kila mwaka kwa miezi miwili nusu ya wanafunzi katika shule ya msingi Mkili kutohudhuria masomo ipasavyo.

Mmoja wa walimu wakongwe katika shule ya msingi Mkili Mwl. John Ntanga anasema kati ya mwezi Januari,Februari na Machi kila mwaka mto huo unapofurika  husababisha  wanafunzi zaidi ya 600 kushindwa kufika shuleni  kutokana na mto kujaa hali ambayo inachangia kuzorotesha kwa elimu.

 “Mto huo ni changamoto kubwa ambayo inachangia utoro katika shule hii,wanafunzi wanaotoka upande mmoja wa mto huo wanashindwa kabisa kuvuka kwa kuwa maji yanajaa hadi juu ya daraja,mto una nguvu kubwa umewahi kusomba gari,wanafunzi hawawezi kuvuka wanakosa masomo’’,alisisitiza.

Ntanga ambaye amekuwa Mwalimu Mkuu katika shule hiyo tangu mwaka 1997 anasema daraja hilo limekuwa kero kubwa kwa kuwa licha ya kujengwa lakini limekuwa linabomoka kutokana na kasi ya maji ya mto huo na kwamba hadi sasa ufumbuzi wake bado haujapatikana.

“Wakala wa barabara TANROAD mara kadhaa wamejaribu kulijenga daraja lakini wakati wa mvua nyingi kati ya mwezi Februari na Machi daraja limekuwa linabomoka na kusombwa na maji kwa hiyo wameamua kuacha kwa sababu ni hasara labda wajenge daraja la juu’’,alisema Ntanga.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wanadai kuwa tatizo la daraja limekuwa ni ahadi ambayo hadi sasa  haijapatiwa ufumbuzi na kuendelea kuwa kero na kwamba wanaamini serikali ya awamu ya tano itatafutia ufumbuzi wa kudumu..

Esau Mwanja anasema eneo hilo ni hatari kwa kuwa magari yanapita ndani ya mto ambapo wakati wa masika ni hatari  kwa kuwa kuna gari ambalo lilisombwa na maji wakati linavuka kwenye mto huo mkubwa ambao maji yake yanakwenda kwa kasi.

Imeandaliwa na Albano Midelo

Afisa Habari Manispaa ya Songea

Mei 9,2018

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa