Mkuu wa Ushirikiano kutoka Ubalozi wa Nchi ya Ujermani DKT. Katrin Bornemann amefanya utalii wa kutembelea makumbusho ya mashujaa ya vita vya Majimaji iliyofanyika jana 04 Agosti 2023 Manispaa ya Songea.
Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kudumisha mahusiano ya kihistoria baina ya Nchi mbili kati ya Tanzania na Nchi ya Ujermani pamoja na kuitembelea familia ya Nduna Songea Mbano.
Dkt. Katrin alisema kuwa pamoja na ujio huo, tarehe 08 mwezi Septemba itakuja timu ya wataalamu kutoka Ubalozi wa Ujermani kutembelea Makumbusho ya Mashujaa wa vita vya Majimaji ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujio wa kiongozi wa Nchi ya Ujermani.” Alibainisha.”
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano, ametoa shukrani kwa Mhe Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro kwa kudumisha mawasiliano na Nchi ya Ujermani ambayo yamepelekea kuja kutembelea makumbusho ya Majimaji na kuongea na familia ya Nduna Mbano Songea. “Alishukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa