Na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI
MANISPAA YA SONGEA.
17.Julai.2022
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameongoza tafrija fupi ya kumpongeza Hamza Masoud Ngose mwanafunzi aliyehitimu masomo yake ya kidato cha sita kwa mwaka 2022 katika Sekondari ya Wavulana Songea, na kuongoza ufaulu katika masomo ya sanaa na kupata Daraja la kwanza 1.3 na hatimaye kuibuka kuwa mshindi wa kwanza kitaifa.
Tafrija hiyo imefanyika hapo 15 Julai 2022 katika shule ya Sekondari ya Wavulana Songea iliyopo kata ya Seedfarm Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, Wilaya, Halmashauri, Wanafunzi, na wadau mbalimbali.
Pololet akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambapo alisema “Miongoni mwa vijana waliokutana na changamoto ya kukosa haki ya kusoma kutokana na sababu ya ulemavu wa kutoona ni Hamza Masoud Ngose, baada ya kutokea changamoto hiyo wazazi wa mwanafunzi huyo walifanya jitihada za kutafuta shule inayoendana na mazingira na alihitimu masomo ya msingi na kujiunga masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari ya Wavulana Songea.”
Aliongeza kuwa baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne alifaulu na kupata daraja la kwanza 1.9 ambapo kwa mwaka 2022 mwezi Mei alihitimu masomo yake ya kidato cha sita ambapo alifaulu na kupata daraja 1.3 kwanza na kuwa wakwanza Kitaifa katika masomo yake ya Sanaa. “Alimpongeza .“
Alisema kutokana na ufaulu wa masomo yote daraja A imewezesha kupanda kwa ufaulu wa shule na kuwa nafasi ya 16 kati ya shule 27 za Sekondari za kidato cha sita Mkoani Ruvuma, nafasi ya 264 kati ya 644 katika shule ambazo zina kidato cha sita.
Halmshauri ya Manispaa ya Songea imemzawadia Hamza Masoud Ngose kiasi cha shilingi 1,000,000, zawadi ya Jina la bweni ambalo litaitwa Hamza Masoud Ngose ambalo linatarajia kujengwa pamoja na zawadi mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, na Chama cha Walimu (CWT).
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inathamini sekta ya Elimu kwa kufanya maboresho ya miundombinu mbalimbali ya elimu ili kuwezesha kuinua kiwango bora cha elimu nchini.
Oddo, ametoa wito kwa wanafunzi wote Mkoani Ruvuma kusoma kwa bidii kama mwanafunzi Hamza Masoud Ngose ambaye ameonesha jitihada za dhati katika kipindi cha masomo na hatimaye kufaulu mtihani wa kidato cha sita na kuongoza kuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa.” Oddo, Alimpongeza.”
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewapongeza walimu pamoja na wanafunzi kwa jitihada walizozifanya katika kufanikisha ufaulu wa mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi mei 2022 ambapo mwanafunzi Hamza Ngose amefanya vizuri na kuongoza kitaifa ambapo alisema kupata ulemavu haimaanishi ukate tamaa ya maisha.
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari ya wavulana Songea Gelalus Gerion Lugome alibainsha kuwa takwimu za maendeleo ya kitaaluma za mwanafunzi zimekuwa zikijipambanua zenyewe kwa ubora wake ambapo kwa mwaka 2019 akiwa kidato cha nne alipata daraja la kwanza akiwa na alama ‘A’sita katika masomo 7 huku akiwa amepata taalma C katika somo kwa njia ya vitendo likiaminika kuathiri ufaulu wake.
Luogome alielleza kuwa, Hamza Masoud Ngose alijiunga na kidato cha tano mwaka 2020 katika kipindi cha masomo yake aliwahi kugombea na kupata ushindi wa kishindo nafasi ya mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi na aliongoza bila pasipo kuathiri malengo ya kitaalma.
Naye mwanafunzi Hamza Masoud Ngose ametoa shukrani kwa uongozi ngazi ya Mkoa, Halmashauri na walimu pamoja na Serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha elimu nchini ambayo imepelekea kufanya vizuri katika mitihani na kupelekea kufaulu kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika masomo ya Sanaa. “Aliwashukuru.”
Aliongeza kuwa kupitia tafrija iliyoandaliwa dhidi yake itamsaidia kufungua fursa za yeye kwenda kusoma elimu ya juu, huku akiiomba Serikali imsaidie kumsomesha ili aweze kutimiza ndoto yake.
Aidha kwa upande wazazi wa Hamza Masoud Ngose wameishukuru Serikali kwa matokeo mazuri ya mtoto wao, pamoja na tafrija fupi iliyoandaliwa na Serikali kwa ajili ya kumpongeza mtoto wao pamoja na zawadi zilizotolewa. “ Walishukuru”
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa