Mwenyekiti wa tume huru ya Taifa mhe. Jaki (Rufaa) Jacobs Mwambegele ametembelea washiriki wa mafunzo ya uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga ambapo amewataka washiriki hao kuwa makini wakati wa mafunzo kwakuwa dhamana waliyopewa ni kubwa hivyo wahakikishe wanafuata maelekezo ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Kauli hiyo imetlewa tarehe 06 januari 2025 alipotembelea washiriki wa uandikishaji yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya wasichana Songea ambapo mafunzo hayo yanalenga uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga ambalo litaanza tarehe 12 januari 2025 hadi 18 januari 2025 ambapo kwa manispaa ya Songea itaandikisha vituo 160 kwa kata 21.
Imeandaliwa na
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa