MWENGE wa Uhuru unatarajia kukimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Juni 7 mwaka huu.Kwa mujibu wa ratiba ya Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Songea unatarajia kupita katika miradi nane ukiwemo mradi wa bwawa la samaki na utalii wa ndani Luhira katika Kata ya Msamala.Mradi huo wa serikali umegharimu zaidi ya shilingi milioni 71.Miradi mingine itakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu katika Manispaa hiyo ni Mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe uliopo kata ya Lilambo,uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga Kata ya Misufini,Uzinduzi wa zahanati ya St.Benjamini Kata ya Msamala,mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mjimwema ambao utawekewa jiwe la msingi.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Mei 27,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa