MWENGE wa Uhuru unatarajia kukimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Juni 7 mwaka huu.Kulingana na Ratiba ya Mwenge jumla ya miradi minane inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa zahanati binafsi ya St Benjamin iliyopo katika Kata ya Msamala. Mwenge wa Uhuru unatarajia kufanya uzinduzi wa zahanati hiyo ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 468.
Miradi mingine ambayo inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa mabwawa ya kisasa ya ufugaji samaki na utalii wa ndani Luhira kata ya Msamala, mradi wa maji Mitendewawa kata ya Mshangano, mradi wa madarasa matatu shule ya msingi Kibulang,oma kata ya Lizaboni, mradi wa kopa ng,ombi lipa ng'ombe kata ya Lilambo, mradi wa kiwanda cha kukoboa mpunga katika Kata ya misufini na mradi wa ofisi ya Kata ya Mjimwema.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa