KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Charles Kabeho amesema miradi yote tisa ya Manispaa ya Songea imekubalika na Mwenge wa Uhuru baada ya kubainika kuwa miradi hiyo ni bora na ina tija kwa wananchi wa Manispaa hiyo.Kabeho ameyasema hayo wakati anazungumza kabla ya Mwenge wa Uhuru kuanza mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Kulingana na Ratiba ya Mwenge wa Uhuru jumla ya miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 945 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru. Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa zahanati binafsi ya St Benjamin iliyopo katika Kata ya Msamala ambao umefanyiwa uzinduzi..
Miradi mingine ni mradi wa mabwawa ya kisasa ya ufugaji samaki na utalii wa ndani Luhira kata ya Msamala, mradi wa maji Mitendewawa kata ya Mshangano, mradi wa madarasa manne shule ya msingi Kibulang,oma kata ya Lizaboni, mradi wa kopa ng,ombe lipa ng'ombe kata ya Lilambo, mradi wa kiwanda cha kukoboa mpunga katika Kata ya misufini na mradi wa ofisi ya Kata ya Mjimwema.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa