Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 18 Tanzania zinazotekeleza miradi ya uendelezaji na uboreshaji wa Miji na Manispaa. (Urban Local Goevernment Strengthening Program).
Ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi unafanyika katika eneo lenye ukubwa wa hekari 15 lilipo katika Kata ya Tanga kilomita 12 toka katikati ya Manispaa ya Songea. Ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi Songea, ulianza tarehe 25/03/2018 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/09/2019. Ujenzi unafanywa na Mkandarasi CHINA SICHUAN INTERNATIONAL CORPORATION (SIETCO) na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri BUREAU FOR INDUSTRIAL CORPORATION (BICO) ambao ni Chuo kikuu cha Dar –es- salaam. Ujenzi huu unahusisha kazi zifuatazo:-
10.Ujenzi wa jengo litakalokuwa na Kituo cha Polisi na Ofisi za uhamiaji
11.Ujenzi wa kisima cha maji safi chenye urefu wa mita 75
12. Kuweka mfumo wa maji safi na maji taka
13. kuingiza umeme wa TANESCO
14. Kuweka Taa za sola
, Mradi huu mpaka kukamilika utagharimu jumla ya Tshs 6,189,340,930.Mpaka sasa Mkandarasi amelipwa kiasi cha Tshs 4,112,445,048.53 ikiwa ni pamoja na malipo ya awali (Advance payment). Gharama za Mhandisi mshauri ni 319,571,801.60 kati ya fedha hizo amelipwa Tshs 180,748,637.51. Utekelezaji wa mradi huu umefikia asilimia 88.
Ujenzi wa kituo kikuu cha Mabasi, umetoa ajira kwa Wananchi 250 Kati ya hao Wataalam ni 41 na wanaobaki ni Wasaidizi mbalimbali waishio katika Kata ya Tanga na Manispaa kwa ujumla hivyo kuongeza kipato kwa Wananchi. Aidha Mradi huu baada ya kukamilika utaisaidia Halmashauri kuongeza bajeti ya mapato ya ndani ya mwaka 2020/2021 toka Tshs 3,749,258,100.00 mpaka Tshs 3,958,478,100.00 sawa na ongezeko la asilimia 5.29. Pia unatarajiwa kutoa ajira kwa Wananchi 396 kwa mchanganuo ufuatao:- madereva na wafanyakazi wa mabasi 306, Wauza maduka 30 Wakatisha Tiketi 60 na Wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo mama lishe na Wamachinga.
Mradi huu baada ya kukamilika utaboresha utoaji wa huduma na utaimarisha usalama wa abiria kutokana na kuwepo kwa kituo cha Polisi na Ofisi za uhamiaji ndani ya kituo cha Mabasi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari Manispaa ya Songea
Septemba 26,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa