KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Charles Kabeho ameridhishwa na viwango vya miundombinu ya zahanati ya Mtakatifu Benjamini iliyopo Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma baada ya kuikagua hivyo amekubali kuizindua ili iendelee kuwahudumia watanzania.Ujenzi wa zahanati hiyo binafsi umegharimu zaidi ya sh.milioni 468.
Hata hivyo Kabeho ameuagiza Mfuko wa Bima ya Afya kutoa kibali haraka ili watanzania waweze kutumia Bima ya Afya kupata matibabu kupitia zahanati hiyo.
Mwenge wa uhuru leo Juni 7 umekimbizwa katika Manispaa ya Songea na kupitia miradi tisa yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 945.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa