Kamati ya siasa ccm Wilaya ya Songea imefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa na serikali ya awamu ya tano ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha mapinduzi (CCM) inayoongozwa na Mh. Rais John Pombe Magufuli, iliyofanyika tarehe 10-11/06/2020 manispaa ya Songea.
Ziara hiyo iliyoongozwa na M/kiti wa CCM Wilaya ya Songea Hamisi Abdallah Ally akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilayani humo ambapo waliweza kutembelea baadhi ya Miradi iliyopo Manispaa ya Songea na Kushuhudia utendaji kazi na usimamizi Bora wa miradi iliyojengwa kwa nguvu za Wananchi na Serikali.
Miongoni mwa Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo ya Siasa ni pamoja na; Ujenzi wa Zahanati ya Likuyufusi ambayo ipo hatua ya kuezekwa, Mradi wa upimaji Viwanja vidogovidogo kata ya Lilambo, Mradi wa Maji Lilambo A na Lilambo B ambao umesanifiwa kuhudumia wakazi wapatao 11,981 kwa Gharama Zaidi ya Tsh Bil 1 ambazo Zimetumika na mradi umeshakamilika, Ujenzi wa zahanati Kata ya Ruhuwiko ambao upo hatua ya ukamilishaji, Mradi wa ujenzi wa kiwango cha lami wa njia ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 1,740 na upana mita 30 ambao uanendelea kujengwa, Ujenzi wa Zahanati ya Makambi Kata ya Ndilimalitembo ambayo ipo hatua ya ukamilishaji, ujenzi wa Barabara ya Tunduru JCT- Seedfarm km 0.75 kwa kiwango cha Lami nyepesi (double surface Dressing) ambao umegharimu bil 33.4 hadi kukamilika, Ujenzi wa daraja la Fataki kwenye barabara ya Songea- Namtumbo ambao bado haujakamilika, Mradi wa Usambazaji wa Umeme wa “REA” Ruhila Seko ( hot line 1.2 km), Kukagua mradi jengo la Maabara na choo Sekondari ya Subira, kuwatembelea Wanufaika wa mradi wa TASSAF Mtaa wa Ruhuwiko Kanisani, pamoja na kukagua vikundi vya wanawake, vijana, na walemavu vilivyowezeshwa kupata mkopo kutoka kwa Mkurugenzi Manispaa kupitia Maendeleo ya Jamii.
Hamisi, akitoa pongezi kwa Mkurugenzi Manispaa ya Songea katika kusimamia vizuri ujenzi wa Miradi hiyo ambayo imefikia hatua nzuri, na ikiwa baadhi ya miradi hiyo kuwa imekamilika na kuanza kutumka, na miradi mingine kunaendelea na ujenzi. Hata hivyo “ alimuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kukamilisha miradi hiyo haraka iwezekanavyo ili kusogeza huduma kwa wananchi ambao hutembea mwendo mrefu kufuata matibabu. Akitaja baadhi ya Zahanati ambazo zinahitaji ukamilishaji wa haraka ni pamoja na Zahanati ya Lilambo, Ruhuwiko, na Makambi.” Alisisitiza.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa