• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI CCM TAIFA DKT MNDOLWA, ATEMBELEA MIRADI MANISPAA YA SONGEA.

Tarehe ya kuwekwa: March 3rd, 2022

Na,

AMINA PILLY,

AFISA HABARI MANISPAA.

03 MACHI 2022.

Mwenyekiti  wa Jumuiya ya Wazazi  CCM Taifa Dkt. Edmund Mndolwa amewataka wanafunzi wote Manispaa ya Songea kuwa na nidhamu pamoja na  kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu masomo yao ipasavyo na  kutimiza ndoto zao.

Dkt. Mndolwa ametoa rai hiyo akiwa Ziarani Manispaa ya Songea alipotembelea miradi ya maendeleo ambayo ni fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo kwa Manispaa ya Songea ilipokea fedha shilingi milioni 660 kwa ajili ujenzi wa vyumba vya madarasa 26  kwa shule ya Sekondari na madarasa matatu shule ya Msingi Shikizi.

Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 03 machi 2022 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo aliweza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa katika kata ya Msamala ambacho kipo hatua ya lipu pamoja na mradi wa ujenzi wa madarasa  katika shule ya sekondari ya Matarawe.

Aidha, akiwa Ziarani hapo, amewataka walimu wote Manispaa ya Songea kutekeleza wajibu wao vizuri  ili waweze kuwasimamia wanafunzi katika masomo yao pamoja na kukagua maendeleo ya kila mwanafunzi ili kukomesha utoro na kushuka kwa ufaulu wa mitihani kwa wanafunzi.

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kusimamia na kuendeleza miradi yote iliyoanzishwa wakati wa uongozi wa Hayati John Pombe Magufuli hususani miundombinu ya umeme, maji, Afya na Elimu.

Alisema Serikali hupanga mipango ya maendeleo kwa kufuata idadi au takwimu , hivyo amewataka wananchi wote wa Manispaa ya Songea  kushiriki zoezi la Sensa ya watu na makazi ambalo linatarajia kufanyika mwaka huu kwa lengo la kupata takwimu ambayo hutumika kupanga maendeleo kwa ngazi ya jamii.

Amewataka wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi Songea Mjini kushiriki katika uchaguzi wa kuwapata viongozi ngazi ya chama (CCM) ambao unatarajia kufanyika  hivi karibuni ambapo alisema kiongozi bora ni yule anayejituma na kutetea haki za wananchi.’Alisisitiza’ 

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Christopher Ngonyani alisema kuwa ujenzi wa kituo cha afya Msamala umetengewa kiasi cha shilingi Milioni 500 ambazo ni fedha kutoka Serikali kuu pamoja na fedha zilizochangwa na wananchi shilingi Milioni 2.5 hivyo kufanya kuwa na jumla ya shilingi Milioni 502,500,000.

Alisema kuwa lengo la kujenga kituo hicho ni kutoa huduma bora na ya karibu kwa wananchi ambapo huduma mbalimbali zitatolewa ikiwemo na upasuaji, upimaji wa VVU, maabara, jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la wodi ya wazazi pamoja na utoaji huduma bora ya afya ya mama na mtoto.

Hadi hivi sasa mradi huo umetumia jumla ya shilingi Milioni 327,469,000 kwa hatua ya plaster na dali ambapo ujenzi huo bado unaendelea. ‘Ngonyani alibainisha’

 Mwisho.

   

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa