NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
28.09.2021
Baraza maalum la Madiwani Manispaa ya Songea limefanya kikao leo tarehe 28 September 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kupitisha hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Kikao hicho kiliongozwa na Mheshimiwa Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Milembe na kuhudhuriwa na Madiwani 28 pamoja na timu ya wataalamu kutoka ndani ya Manispaa ya Songea.
Akiwasilisha taarifa ya hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Muhazina wa Manispaa Emmanuel Mgaya alisema kuwa taarifa hiyo imeandaliwa kwa mujibu Memoranda ya fedha ya mwaka 2009 sehemu ya IV agizo namba 24 mpaka 32, waraka wa bodi ya wahasibu na wakaguzi Tanzania, sheria ya fedha ya Serikali za mitaa 1982 kifungu namba 40, kanuni za uandaaji hesabu za umma za kimataifa, pamoja na miongozo ya TAMISEMI juu ya uandaaji na uwasilishaji wa hesabu za Halmashauri kwa mwaka 2020/2021.”Alibainisha”
Mgaya alieleza kuwa taarifa ya hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Songea imetolewa kwa kuzingatia taarifa ya Mizania ( Statement of Financial position), taarifa ya mapato na matumizi (Statement of Financial performance), taarifa ya mtiririko wa mapato, mwenendo wa mali na mtaji, taarifa ya ulinganifu wa bajeti dhidi ya matumizi halisi ( Statement of comparison of budget and actual amount) pamoja na maelezo ya hesabu.
Taarifa hiyo ya hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ilipokelewa na kupitishwa na baraza la madiwani kwa asilimia 100%.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa