Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Mirembe Diwani wa kata ya Bombambili ameanza Ziara jana ya kutembelea mitaa 5 mitano iliyopo kwenye kata yake ya Bombambili na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuongea na wananchi na kutoa shukrani kwa wananchi baada ya kushinda uchaguzi.
Ziara hiyo imeanza jana tarehe 23 juni 2021 ambayo inatarajia kukamilika 27 juni 2021 kwa lengo la kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuishirikisha jamii juu ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi.
Jeremiah alisema “ Kiongozi bora ni yule anayependa kukosolewa na kujifunza kutoka kwa jamii anayoiongoza, hivyo ameawataka wananchi hao kuendela kuleta ushirikiano katika kuleta maendeleo na sio kuanzisha migogoro.
Alisema kwa muda mfupi baada ya kuingia madarakani ameweza kutatua baadhi ya changamoto mashuleni ikiwemo na za upungufu wa madarasa Shule ya msingi Mputa na matundu ya vyoo ambapo wamejenga madarsa 3, ujenzi wa madarasa mawili 2 Shule ya Msingi Tembo, ujenzi wa madarasa ya 3 ya Shule ya Msingi Bombambili, Ujenzi wa madarasa 5 shule ya Sekondari Bombambili fedha shilingi milioni 80,000,000/ kutoka Mkurugenzi Manispaa.
Alibainisha kuwa mafanikio yote yanayopatikana kwenye kata yake juu ya kufanikisha kutatua baadhi ya changamoto mbalimbali kwenye kata ya Bombambili zinatokana na ushirikiano mzuri na Mh. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kuiwezesha kata hiyo kupata fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa, vyoo, barabara na zahanati. " Alimpongeza".
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kutatua changamoto za miundombinu ya barabara za mitaa ambayo husimamiwa na TARURA ambapo amewataka wananchi hao kuleta ushirikiiano wakati wa utekelezaji wa zoezi la matengenezo ya barabara za mitaa na kuachana na tabia ya kuzuwia / kusababisha migongano.
Amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kujisajili kwenye huduma ya mfuko wa Bima ya afya iliyoboreshwa ambayo huchangiwa kwa shilingi 30,000 kwa kaya isiyozisi watu 6.
Naye Diwani wa Viti maalum Anna Mlimira alisema moja ya majukumu yake ni kuhakikisha anahamasisha wananwake, vijana na walemavu kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa fedha zitokanazo na mapato ya ndani 10% (wanawake 4%, Vijana 4, na walemavu 2%.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
24 juni 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa