MBUNGE wa Jimbo la Nyasa ambaye pia na Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi.Stella Manyanya amemkabidhi Afisa Mtendaji wa kata ya Mpepo Raphael Mapunda pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kufuatilia miradi ya maendeleo na ukusanyaji mapato katika kata ya mpepo .
Amemkabidhi pikipiki hiyo katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa na kushudiwa na Ofisa Mipango Wilaya ya Nyasa Jabir Chilumbana viongozi wa chama cha Mapinduzi na watumishi wengine wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
Akizungumza wakati anakabidhi pikipiki hiyo,Manyanya amesema mfuko wa Jimbo umeona una kila sababu ya kuboresha miundombinu ya usafiri kwa watendaji ili waweze kufanya kazi zao kwa juhudi na maarifa na kuwahudumia wananchi kwa kufuatilia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya Nyasa.
“Mfuko wa Jimbo umeona unakila sababu ya kukuwezesha Afisa mtendaji wa kata ya Mpepo kutokana na jiografia ya kata yako vijiji vyako vimekaa mbalimbali hivyo unapata shida ya utendaji kazi wa kufuatilia miradi ya maendeleo na ukusanyaji mapato hivyo tunaomba uongeze juhudi ili uweze kufikia malengo uliyojiwekea na uliyopangiwa na Halimashauri”
Akipokea Pikipiki hiyo ofisa mtendaji wa Kata ya mpepo aliahidi kuitunza na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa awali alikuwa hana usafiri hivyo yeye na wataalam wake walikuwa wanapata shida ya kufuatilia miradi ya maendeleo iliyopo katika kata ya mpepo Wilayani hapa,Hivyo kwa sasa ataifikia miradi yote ya maendeleo na kuhamasisha maendeleo katika Vijiji vyake vyote.
Imeandaliwa na Netho Credo
Afisa Habari wa wilaya ya Nyasa
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa