NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege yupo mkoani Ruvuma.
Akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kandege amekagua miradi ya ujenzi wa stendi ya kisasa na machinjia katika Kata ya Tanga,mradi wa kituo cha Afya kata ya Ruvuma na mradi wa barabara za lami mjini Songea
Mara baada ya ukaguzi wa stendi ya mabasi, Naibu Waziri ameridhishwa na hatua ya ujenzi unaofanywa na Kampuni ya China Sichuan International.mradi umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2018.Mradi katika awamu ya kwanza unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikia asilimia 14.
Kazi ambazo zinafanyika awamu ya kwanza katika stendi hiyo ni ujenzi wa lami nzito yenye kilometa mbili,taa barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya tiketi,jengo la utawala,vyoo vya matundu 12 na eneo la kupaki magari.Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 444.
mradi hadi kukamilika unatarajia kugharimu shilingi bilioni 12 ambapo katika awamu ya kwanza, zitatumika shilingi bilioni sita na kwamba stendi mpya ya mabasi inatarajia kuanza kazi baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji ambayo ni kuanzia Oktoba 2019.
Ili kuendana na kasi ya ukuaji wa mji,Manispaa iliamua kutenga eneo la kujenga kituo kikuu cha mabasi kuwa Kata ya Tanga ikiwa ni umbali wa takribani kilometa 14 toka mjini Songea.Kazi nyingine ambazo zitafanyika katika awamu ya kwanza na pili ya mradi huo kuwa ni kujenga barabara za kuingia na kutoka stendi zenye kiwango cha lami nzito,kujenga mirefeji ambayo itapeleka maji mtoni,ujenzi wa eneo la stendi lenye ukubwa wa meta za mraba 32,914,kuweka taa za barabarani katika eneo lote la stendi,eneo la utawala na kujenga majengo yenye hoteli za kisasa.
Fedha za mradi wa stendi zimetolewa kupitia Benki ya Dunia,jumla ya hekari 15 zimetwaliwa katika eneo hilo ili kupitisha stendi,ambapo shilingi milioni 38 tayari zimelipwa kama fidia kwa wananchi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 11,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa