Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Izack Kamwele ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mbinga –Mbamba-bay unaoendelea katika eneo la mbamba-bay nangombo na hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu unaounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe.
Aliyasema hayo jana(tarehe 09.10.2018) wakati akiongea na waandishi wa habari katika eneo la chunya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kwenye kiwanda cha kusaga mawe kwa ajili ya kokoto wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba-bay yenye urefu wa kilomita 67 ambayo ujenzi wake umeanza katika eneo la Mbamba-bay hadi Nangombo ambapo barabara hiyo inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 129..
Waziri alifafanua kuwa ameridhishwa na ujenzi wa barabara hiyo jinsi unavyoendelea na maandalizi yake na kumtaka mkandarasi afanye kazi kwa juhudi kubwa na maarifa ili kazi iendelee kwa nguvu zote ili kuwapa wananchi fursa ya kuwa na barabara nzuri watakayoitumia katika shughuli zao za kiuchumi.
Aliongeza kuwa tangu asubuhi alikuwa akitembelea miradi inayotekelezwa katika mkoa wa Ruvuma hususani alikagua barabara ya Likuyufusi –mkenda ambayo alisema upembuzi yakinifu ulishafanyika lakini kutokana na ugunduzi wa makaa ya mawe katika eneo la Muhukuru wamelazimika kufanya tena upembuzi huo kwa kuwa magari mengi yenye uzito mkubwa yatapita katika barabara hiyo na barabara ya kitai-lituhi na lituhi-mbamba-bay pamoja na kukagua daraja la mto Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe.
“Ndugu wanahabari nimekuwepo tangu asubuhi nikiwa nakagua miradi ya maendeleo na hii leo nimekagua barabara ya Likuyufusi –Mkenda ,kitai-Lituhi na Lituhi-Mbamba-bay na Mbamba-bay-mbinga kwa kifupi na ujenzi wa barabara ya mbinga-Mbamba-bay kwa kuwa maandalizi yake na mazuri na hata kasi ya ujenzi ni nzuri na inaendelea vizuri Lakini Sijaridhika na ujenzi wa Daraja la mto nimeridhishwa Ruhuhu kwa kuwa Mkandarasi huyo ni Mtanzania lakini hana uwezo wa kujenga lile Daraja.Nimeongea nae mkandarasi anayejenga daraja na sijataka nitoe amri ya kuwachisha kazi lakini nimemshauri aonane na wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Ruvuma ili akabidhi yeye mwenyewe ile kazi ili iweze kukamilika kwa muda wa miezi miwili kwa kuwa kazi iliyobaki siyo kubwa sana.”
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba alimpongeza waziri huyo kwa mikakati ya ujenzi wa barabara hizo na kusema kuwa kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa anaishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kwa kujenga Barabara za huku mpakani mwa Tanzania kwa kuwa barabara ya Lituhi Mbamba-bay iko karibbu mpakani mwa tanzani na malawi upande wa Tanzania hivyo itasaidia sana katika ukuaji wa uchumi kwa wakazi wa Wilaya ya Nyasa.
Katika hatua nyingine amefurahi kuona rasilimali ya makaa ya mawe iliyopo katika mkoa wa Ruvuma Muhukuru Wilayani Songea pamoja na Ruanda Wilayani Mbinga kwa kuwa ni vichocheo vya ukuaji wa sekta ya Viwanda kwa kuwa Viwanda vingi vinatumia makaa ya mawe na akavitaja viwanda hivyo kuwa ni cha Dangote Mtwara na viwanda vya simenti cha Tanga na Dar es salaam na viwanda vingine vya nchi jirani za Rwanda na Kenya.
IMEANDALIWA NA
NETHO C. SICHALI
AFISA HABARI
NYASA DC
09 Octoba,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa