WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako amewataka wazazi nchini kuwahimiza watoto kusoma masomo ya sayansi ili kuongeza idadi ya wahandisi watakaofanya kazi katika sekta mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kongamano la nne la wahandisi wanawake lililofanyika jijini Dar es Salaam, Profesa Ndalichako pia amewataka wanafunzi kutoogopa somo la hesabu kwa kuwa ndiyo msingi wa kufanya vizuri katika maeneo mengi ya kazi.
Amesema sekta ya uhandisi inafanya kazi kubwa katika kukuza uchumi kupitia miradi licha ya uwepo mdogo wa wahandisi katika fani hiyo hususani wanawake, jambo alilosema ni vyema likajengewa msukumo kuanzia ngazi ya wazazi.
“Wazazi mna jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wanafanya vizuri katika masomo, hususani ya sayansi ili kuwawezesha kuwa wahandisi wazuri hapo baadaye, bila ushawishi wa wazazi katika eneo hilo bado tutaendelea kupata idadi ndogo wa wanafunzi wanaosoma sayansi,” amesema Profesa Ndalichako.
Amesema, Serikali kupitia wizara hiyo ya elimu inaendelea kufanya maboresho katika sekta ya elimu ikiwemo kuongeza vitabu vya sayansi na ujenzi wa maabara kwa lengo la kufanikisha mpango wa kuwapata wahitimu wa kutosha katika masomo ya sayansi.
Mwenyekiti wa Chama cha wahandisi wanawake Alice Isibika, mbali na kutaja mafanikio yaliyofikiwa na chama hicho tangu kuanzishwa kwake, alisema changamoto inayowakabili kuwa ni pamoja na idadi ndogo ya waandisi wanawake katika maeneo mbalimbali.
Alisema katika idadi ya wahadisi zaidi ya elfu ishirini waliosajiliwa na bodi ya wahandisi nchini(ERB),wanawake ni asilimia kumi pekee hatua aliyosema kuwa kwa kiasi kikubwa inadhohofisha nguvu za wanawake katika ujenzi wa Taifa.
CHANZO NI https://habarileo.co.tz/habari/2018-08-045b658a379f35f.aspx
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa