AFISA Maliasili na utalii wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma, Bugingo Bugingo amesema utafiti umebaini kuwa ndege ambao wanazaliana katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wilayani Makete Mkoani Njombe, wanaposafiri kutoka au kwenda Ulaya na nchi nyingine za Afrika wanapumzika maeneo ya wilaya ya Nyasa kwa ajili ya kujipatia chakula cha aina mbalimbali katika mwambao mwa ziwa Nyasa ukiwemo msitu wa Ruhekei.
Bugingo alikuwa anatoa taarifa katika tamasha la wiki ya utalii katika wilaya ya Nyasa kwa Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya katika kijiji cha Kihagara.
Imetolewa na Albano Midelo
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa