OFISI ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma jana iliitisha mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya nguruwe kujadili mkakati wa kuzuia maambukizi ya ugonjwa na namna ya kudhibiti ueneaji wa homa ya nguruwe.
Mkutano huo umeshirikisha wadau toka Halmashauri tatu za mkoa wa Ruvuma ambazo zina ugonjwa wa homa kali ya nguruwe (African Swine Fever).
Halmashauri hizo ni Manispaa ya Songea,Halmashauri ya Nyasa na Halmashauri ya wilaya ya Songea.
Kwa mujibu wa Afisa mifugo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,Bilaly Mwegeni,uchinjaji nyama ya nguruwe umeruhusiwa kufanyika chini ya usimamizi maalum na kwamba uchinjaji utafanyika katika vituo maalum ambavyo ni Songea Girls,Msamala na Lizaboni.
Amesema kwa siku tatu wanakagua vituo hivyo na kwamba uchinjaji rasmi unatarajia kuanza kabla ya Machi 30 mwaka huu.takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa wa homa kali ya nguruwe tangu Januari 31 hadi Machi 14 umeua zaidi ya nguruwe 864 katika Manispaa ya Songea hali ambayo ilisababisha kusitisha uchinjaji .
Taarifa imetolewa na Abano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa